Mamelodi Sundowns yawagonga Petro De Luanda mabao 2-0 AFL

LUANDA-Klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imefanikiwa kutwaa alama tatu zikisindikizwa na mabao 2-0 katika mchuano wa Robo Fainali ya Ligi ya Soka barani Afrika (African Football League-AFL).

Mamelodi Sundowns wakiwa wageni katika Dimba la Estádio 11 de Novembro jijini Luanda nchini Angola wametembeza kichapo hicho kwa Petro De Luanda ambao walikuwa nyumbani.

Katika mtanange huo ambao umepigwa leo Oktoba 21, 2023 dakika ya 67 kiungo mshambuliaji Marcelo Iván Allende Bravo wa Mamelodi Sundowns alitikisa nyavu za wenyji hao.

Baada ya kiungo huyo wa Kimataifa kutoka nchini Chile kuzitikisa nyavu hizo, bao hilo lilikuja kuongezwa nguvu na mshambuliaji Thapeo Maseko dakika ya 80 kwa kuzitikisa nvavu hizo tena.

Mtanange huo ambao ulionekana kuwa na mvuto wa aina yake uliongozwa na mpuliza kipenga Ibrahim Mutaz kutoka nchini Libya akisaidiwa na Khalil Hassani kutoka nchini Tunisia na Ahmed Hossam Taha kutoka nchini Misri.

Vijana wa Kocha Alexandre Santos na Rulani Mokwena wanatarajiwa kurudiana tena Oktoba 24, 2023 ambapo matokeo hayo yataamua ni nani atakutana na mshindi wa jumla kati ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam na Al Ahly ya Misri.

Oktoba 20, 2023 Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam iliandika historia mpya ya soka baada ya kutunishiana misuli na miamba wa soka Al Ahly ya Misri katika uzinduzi wa michuano hiyo ya African Football League (AFL).

Ni kupitia mtanange wa nguvu ambao ulipigwa katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Simba SC ambao walikuwa ni wenyeji katika mchezo huo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) walikuwa wa kwanza kuifungua michuano hiyo mipya barani Afrika huku wakitoka sare ya mabao 2-2.

Mabao ya Al Ahly yalifungwa na Reda Slim dakika ya 45+1 na Mahmoud ‘Kahraba’ Soliman dakika ya 63, wakati ya Simba SC yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 53 na Sadio Kanoute dakika ya 59.

Aidha, klabu hizo zitarudiana Jumanne katika Dimba la Cairo International nchini Misri na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Petro de Luanda ya Angola na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news