Mradi wa UNESCO-ALWALEED PHILANTHROPIES wazinduliwa

ZANZIBAR-Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya ZanzibarMhe. Tabia Mwita Maulida mezindua Mradi wa UNESCO-ALWALEED PHILANTHROPIES unaolenga kukuza Maendeleo ya kijamii kupitia Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) na ajira zinazohusiana na Utamaduni.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo mjini Zanzibar,Oktoba 24, 2023amesema mradi huo utasaidia kutoa elimu ya kulinda Utamaduni pamoja na wadau wa Utamaduni kunufaika na bidhaa za Utamaduni.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Nicholas Mkapa amesema mradi huo utanufaisha vijana katika Utengenezaji wa Filamu, Muziki na Sanaa kwa kukuza uchumi na kuwawezesha vijana kupata kipato.

Aidha, mwakilishi wa UNESCO hapa nchini Dkt. Michael Toto amesema lengo la Mradi huo ni kukuza maendeleo ya jamii ya Tanzania kwa kutoa elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi na ajira zinazotokana na Utamaduni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news