Msigwa:BAKITA ibueni vyanzo vipya vya mapato

DAR ES SALAAM-Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa ametembelea Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na kuiagiza menejimenti ya baraza kuibua vyanzo vipya vya mapato ikiwa ni pamoja na kuanzisha vituo vya Kiswahili jijini Dodoma na Arusha.

Katibu Mkuu Msigwa ameyasema hayo Oktoba 12, 2023 katika ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara hiyo, ambapo ameitaka kuanzisha kozi fupi kwa Waandishi wa Habari, Makatibu Muhtasi na Watanzania kwa ujumla.

“Hii ni ziara ya kutembelea taasisi ambazo ziko chini ya wizara ninayoiongoza ili nijue maendeleo yake na kubadilishana mawazo na viongozi wa taasisi,"amesema Msigwa.
1000336995
“Tutabidhaisha Kiswahili na tutasimamia Kiswahili fasaha kwa kuwa tunayo fursa ya kupeleka Kiswahili katika nchi zote duniani. Kati ya mambo yasiyofaa ni kuona vyombo vya habari vinaharibu lugha ya Kiswahili, tushirikiane na BAKITA kutumia Kiswahili fasaha kwani sisi ndio wa kushika bendera yetu na kuipeperusha lugha fasaha ya Kiswahili,"amesema Bw. Msigwa.
1000336993
Amelitaka BAKITA kuongeza jitihada za kutangaza lugha ya Kiswahili kwani ndilo jukumu lake la msingi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news