Prof.Muhongo awaunga mkono wanakijiji Kwikerege

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoa wa Mara, Prof. Sospeter Muhongo ameunga mkono juhudi za wananchi wa Kijiji cha Kwikerege kilichopo katika Wilaya ya Musoma walioamua kujenga zahanati ya kijiji chao ambapo ameanza kwa kutoa mifuko 100 ya saruji.

Ni katika harambee ambayo Prof.Muhongo ameifanya ya kuchangia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji hicho akiwa ameambatana na Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Vijijini chini ya Mwenyekiti wake, Denis Ekwabi.

Aidha, Prof. Muhongo amewataka wananchi wa kijiji hicho kuongeza kasi ya ujenzi wa zahanati hiyo huku akisema kuwa yuko nyuma yao katika kuhakikisha zahanati hiyo inakamilika mapema.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma Vijijini, Denis Ekwabi amepongeza hatua ya wananchi hao huku akisema kuwa afya bora ni muhimu kwa ajili ya maendeleo, hivyo hatua waliyoichukia ina manufaa makubwa.

Kwa upande wao wananchi wa kijiji hicho, wamempongeza Prof. Muhongo kwa kuunga mkono juhudi zao na ushirikiano wake wa kuchangia maendeleo.

Wamesema, hatua ambayo itasaidia waweze kupata huduma za afya karibu na makazi yao pindi itakapokamilika kwani kwa sasa wanalazimika kutembea umbali wa kilometa tano kwenda kufuata huduma za afya kijiji jirani cha Rusoli.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Oktoba Mosi, 2023 imebainisha kuwa "Kijiji cha Kwikerege ni moja ya vijiji vitatu (3) vya Kata ya Musanja,

"Kijiji hiki hakina zahanati, kwa hiyo wakazi wake wanapohitaji Huduma za Afya wanalazimika kutembea umbali usiopungua kilomita tano (5) kwenda kwenye Zahanati ya Kijiji jirani cha Rusoli. Hivyo Wananchi wameamua kujenga Zahanati ya kijiji chao," imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

HALI YA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA JIMBONI MWETU (MUSOMA VIJIJINI) IKO HIVI.

"Vituo vya Afya sita.Baadhi, vipya, vinasubiri kupewa wafanyakazi na vifaa tiba. Zahanati ni 44, ambapo 24 za Serikali na nne za binafsi huku 16 zinajengwa,"imeeleza taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news