Rais Dkt.Mwinyi:Zanzibar imeanzisha Mpango wa Uwekezaji wa Sekta ya Maji

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ilianzisha mpango wa uwekezaji maji wa mwaka 2022 hadi 2027.
Ni mpango uliolenga kukusanya rasilimali kwa ajili ya uwekezaji salama wa maji kwa utekelezaji endelevu wa muda mrefu wa usambazaji maji kwa mahitaji ya msingi na kiuchumi.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Oktoba 25,2023 alipofungua kongamano la 24 la maji linaloshirikisha mataifa kutoka Mashariki na Kusini mwa Afrika katika Hoteli ya Verde Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa mpango huo umezingatia maeneo matano yakiwemo uwekezaji wa maji na fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za maji na usafi wa mazingira, kujenga uwezo wa kuhimili hali hewa.

Sambamba na usawa wa kijinsia na ushirikishwaji wa kijamii, kuimarisha utaratibu wa kitaasisi pamoja na uchumi wa buluu na usimamizi endelevu wa rasilimali maji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news