Ruksa kwa vyombo vya habari vya kujitegemea na wanahabari

DODOMA-Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi amesema ni ruksa kwa Vyombo vya Habari vya kujitegemea na Waandishi wa Habari kutoa taarifa na matangazo yanayohusu Serikali.
Amesisitiza kuwa,takwa hilo ni kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari Sura 229 na Marekebisho yake ya Mwaka 2023.

Matinyi amesema hayo baada ya taarifa kuenea mitandaoni zikiihusisha Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro ikisema ni kosa kisheria kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (1) (b), (iv) cha Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 kwa Chombo cha Habari binafsi au Mwandishi wa Habari kuzungumza masuala mbalimbali ya Serikali (National Issues) bila idhini au mwongozo wa Serikali.

“Hilo siyo sahihi. Sheria imeweka bayana haki za msingi za Vyombo vya Habari na Waandishi wa Habari ambazo ni kutafuta, kuchakata na kutangaza au kuchapisha habari. Waandishi wanaruhusiwa isipokuwa kwa taarifa ambazo zimezuiliwa kwa mujibu wa sheria,”amesema Matinyi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news