Serikali yawataka wananchi kutunza vyanzo vya maji

MBEYA-Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji ili viwanufaishe na kuhifadhi mazingira.
Amesema hayo wakati akizungumza na wananchi akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua Mradi wa Kuhifadhi Ardhi (SLM) katika Bonde la Ziwa Nyasa wilayani ya Ludewa mkoani Mbeya.

Naibu Waziri Khamis, amesema shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zinazofanyika kupitia mradi huo zikiwemo ufugaji wa samaki ni matunda ya uwepo wa vyanzo vya maji

Amesema Wilaya ya Ludewa na Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa maeneo yenye vyanzo vingi vya maji hivyo ametoa rai kwa viongozi kuhakikisha vyanzo hivyo vinatunzwa.

“Ndugu zangu Mwenge wa Uhuru si umepita huku kwenu?…na mmeona ujumbe wake ulihimiza namna ya kutunza mazingira na kuhifadhi vyanzo vya maji sasa leo hii yale mabwawa ya samaki yasingekuwepo kama tusingekuwa na vyanzo vya maji, leo hii nimepita kule nimeona mnafanya kilimo cha irrigation yanafanyika haya kwasababua tuna vyanzo maji, tuvitunze,” amesema.

Naibu Waziri Khamis amewataka wananchi kuwa walinzi wa vyanzo vya maji vitunze ili wanufaike kinyume na hapo watakuwa wanategemea tu mvua inyeshe ndipo wapate maji.

Sanjari na vyanzo vya maji, pia Khamis amewataka wananchi kuitunza miradi hiyo walioyonufaika nayo ikiwemo kupanda miti kwa wingi ili iwanufaishe.

Amewatahadharisha wananchi kulinda amani iliyopo kuepuka madhara yanatokana na migogoro mbalimbali inayoweza kujitokeza endapo amani itachezewa.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Lugarawa, Erasto Mhagama akizungumzia mradi wa ufugaji wa samaki unaotekelezwa kupitia SLM katika kata hiyo ameshukuru Serikali kwa kuwapelekea mradi huo katika wilaya yao.

Ameiomba Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inayotekeleza mradio huo chini ya ufadhili wa Mfuko Mazingira wa Dunia (GEF) kuongeza wigo wa utekelezaji wa mradi ili uwafikie wananchi wnegi zaidi.

Nae Longinus Mgani ambaye ni mwenyekiti wa Kikundi cha INAWEZEKANA kinachojishughulisha na mradi wa ufugaji wa samaki amesema wameitumia fursa ya mradi kujikwamua kimapato.

Amesema kuwa mradi huo umewapa hamasa ya kuacha kufanya shughulli za kilimo cha kuhamahama kisicho endelevu na kukata miti ambazo husababisha uharibifu wa mazingira.

Mradi wa Kuhifadhi Ardhi (SLM) katika Bonde la Ziwa Nyasa unatekelezwa katika halmashauri za wilaya tano zikiwemo ya Kyela (Mbeya), Makete na Ludewa (Njombe), Mbinga na Nyasa (Ruvuma).

Lengo la mradi, pamoja na kuhifadhi ardhi katika eneo hilo lakini pia kuisaidia jamii kufanya shughuli za kujipatia kipato bila kuathiri mazingira na kulinda hifadhi ya Bonde la Ziwa Nyasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news