TARURA YAENDELEZA UBABE KWA KUIPIGA ARDHI 1-0

IRINGA-Timu ya Mpira wa miguu ya TARURA yaendeleza ubabe kwa siku tatu mfululizo ambapo leo imefanikiwa kuipiga Ardhi goli 1-0 kwenye mashindano ya SHIMIWI.
Katika mchezo wa leo uliochezwa kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Mkwawa,TARURA ilifanikiwa kuona goli la ardhi katika kipindi cha kwanza dakika ya 28 ambapo mchezaji Erick Tegamaisho aliipatia goli la ushindi.

Hadi mwisho wa mchezo huo timu ya Ardhi haikufanikiwa kuliona goli la TARURA licha la mchezaji wa TARURA, Makunge Mwera kupewa kadi nyekundu.
Hadi leo TARURA inaongoza kwa kuwa na pointi 9 na magoli 8 ambapo katika mechi ya kwanza dhidi ya Wakili Mkuu iliibuka kidedea kwa magoli 4-0 na katika mechi ya pili dhidi ya Wizara ya Elimu ilitoka mshindi kwa 3-2.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news