Umoja wa Mataifa (UN) kuadhimisha miaka 78 ya kuanzishwa kwake

DAR ES SALAAM-Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania unatarajia kuadhimisha miaka 78 tangu ilipoanzishwa mwaka 1945.
na waandishi wa Habari kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Noel Kaganda amesema maadhimisho ya miaka 78 ya Umoja wa Mataifa yatafanyika tarehe 24 Oktoba 2023 katika viwanja vya Karemjee jijini Dar es Salaam.

Balozi Kaganda amesema wakati UN ukiadhimisha miaka 78 tangu kuanziswa kwake, Tanzania inajivunia kuwa mwanachama wa Umoja huo na imekuwa ikifanya vizuri katika baadhi ya maeneno ya malengo ya maendeleo endelevu hususan katika masuala ya chakula, elimu, jinsia, nishati, maji, amani na usalama.

Balozi kaganda aliongeza kuwa Tanzania inajisikia fahari kama mwanachama wa UN kwa kusimamia kikamilifu misingi ya Umoja huo na kuendelea kutoa mchango wake katika kutekeleza malengo adhimu.
Kwa upande wake Mratibu Mkazi wa UN Tanzania, Bw. Zlatan Milišić alisema Umoja wa Mataifa unafurahia kuadhimisha miaka 78 tangu kuanzishwa kwake na miaka 62 ya ushirikiano kati yake na Tanzania ambapo wakati wote zimekuwa na uhusiano mzuri na imara na Tanzania imekuwa ikichangia kikamilifu katika kuchagiza ajenda ya maendeleo ya kimataifa, katika kuandaa na kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Maadhimisho ya mwaka huu yataongozwa na kaulimbiu isemayo “Kuwekeza leo kwa ajili ya kesho kwa kuinua vijana wa Kitanzania”. Maadhimisho hayo yataongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki, (Mb.).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news