Askari wanawake wapewa somo

DAR ES SALAAM-Askari wanawake nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kushiriki misheni za kulinda amani katika mataifa yenye changamoto za kiusalama.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya 23 ya Azimio la 13-25 ambalo linalenga kuwashirikisha askari wanawake katika misheni za ulinzi wa amani.

Akiongea katika maadhimisho ya 23 ya ulinzi wa amani yaliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania jijini Dar es Salaam, Mwakilishi wa UN Women Tanzania, Bi.Hodan Addou amesema, lengo la Umoja wa Mataifa ni kuwashirikisha askari wanawake katika misheni za ulinzi wa amani.

Pia,amebainisha kuwa katika misheni za ulinzi wa amani kumekuwepo na changamoto kubwa kwa makundi ya wanawake na watoto.

Ameeleza kuwa, wahanga wakubwa katika machafuko ya kiusalama yanapotokea ni wanawake na watoto huku akisema Umoja wa Mataifa utaendelea kuweka mazingira bora ya kiusalama kwa makundi hayo.

Kwa upande wake Kamishina wa Utawala na Rasilimali Watu wa Jeshi la Polisi, CP Suzan Kaganda amesema, changamoto kubwa iliyokuwepo siku za nyuma kwa askari wanawake ni uthubutu na utayari wa ushiriki wa askari wa kike katika ulinzi wa amani.

ACP Kaganda amebainisha kuwa, kwa sasa askari wanawake wamekuwa wakishiriki misheni za ulinzi wa amani kutoka na elimu na kupata kipaumbele na mafunzo ya ulinzi wa amani.

Kwa upande wake Balozi wa Swizerland, Didier Chassot amesema, katika maswala ya ulinzi wa amani lazima waangalie usawa wa kijinsia ili misheni hizo ziwe na matokeo chanya kwa makundi yote huku akiwaomba kuendelea kuweka mazingira bora ya misheni za kulinda amani.

Kwa upande wa uongozi wa kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani umesema, umeongeza nafasi za udahili kwa askari wanawake katika mafunzo ili kuongeza uwakilishi wao katika misheni mbalimbali za Umoja wa Mataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news