Saudi Arabia yaungwa mkono kuandaa Kombe la Dunia 2034

JEDDAH-Takribani mataifa 90 hadi sasa yameunga mkono nia ya Saudi Arabia kuandaa Kombe la Dunia la 2034.

Vyama 12 vya mwisho vilivyotangaza uungwaji mkono wao ni mashirikisho ya soka ya Tanzania, The Bahamas, Montserrat, Visiwa vya Virgin vya Marekani, Haiti, Guyana, Suriname, Zambia, Gabon, Eritrea, Cambodia, na Ugiriki. Ugiriki ni nchi ya nne barani Ulaya kuunga mkono ombi la Saudia.

Shirikisho la Soka la Saudi Arabia (SAFF) tayari limewasilisha barua ya nia (LOI) na kutia saini tamko kwa FIFA kuwasilisha ombi la kuandaa Kombe la Dunia la FIFA 2034.

Saudi Arabia ilitangaza kwa mara ya kwanza nia yake ya kutoa zabuni kwa toleo la 2034 la michuano hiyo Oktoba 4, na barua ya nia iliyotiwa saini na Rais wa SAFF, Yasser Al Misehal inathibitisha dhamira ya Ufalme ya kuanza mchakato wa zabuni uliowekwa na FIFA.

Chini ya wiki moja baada ya SAFF kutangaza nia yake ya kutoa zabuni kwa Kombe la Dunia la FIFA,zaidi ya vyama 90 Wanachama wa FIFA kutoka katika mabara tofauti wameahidi hadharani kuunga mkono Ufalme.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news