Azma ya kuifungua Pemba kiuchumi inakwenda vizuri-Rais Dkt.Mwinyi.

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, wakati wa kuadhimisha miaka mitatu ya uongozi wake azma yake ya kuifungua Pemba kiuchumi inakwenda vizuri.
Dkt.Mwinyi aliahidi kuifungua Pemba kibiashara na uwekezaji kupitia maeneo makuu manne ikiwemo mkakati wa kuboresha bandari za Pemba ambao unaendelea, ujenzi wa barabara, kuvutia uwekezaji wa viwanda eneo la Chamanangwe yote yatatimia kabla ya uchaguzi mkuu 2025.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati akizindua boti mpya ya Zanzibar 3 ya Kampuni ya Zan Fast Ferries itakayofanya safari zake Pemba hadi Unguja kwa muda wa saa mbili, Tanga na Dar es Salaam.

Mheshimiwa Rais amefanya uzinduzi huo Novemba 1, 2023 katika Bandari ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba

Rais Dk.Mwinyi amesema, alizungumza na wawekezaji mbalimbali kuhusu changamoto ya usafiri Pemba wa anga na bahari hatimaye wawekezaji hao wameitikia wito ikiwemo Kampuni ya Azam Marine, na tayari Zan Fast Ferries wameleta boti mpya ya Zanzibar 3 kwa safari za Pemba. Pia kampuni za Flight link na Assalam Air kuongeza ndege kwa safari za Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news