BoT yaishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

DAR ES SALAAM-Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mchango wake katika kuwezesha utekelezaji wa sera ya fedha.

Hayo yamesemwa Novemba 13, 2023 na Naibu Gavana, Bi. Sauda Msemo wakati wa ziara ya Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Katika ziara hiyo iliyofanyika katika Ofisi za BoT Dar es Salaam, kamati ilipata fursa ya kujifunza kuhusu jukumu la msingi la BoT ambalo ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara.

Majukumu mengine ya BoT ni pamoja na kutoa sarafu ya nchi, kusimamia mabenki na taasisi za fedha, kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo nchini, kuhifadhi akiba ya nchi ikiwemo fedha za kigeni na dhahabu; kutoa ushauri wa masuala ya kiuchumi na fedha kwa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news