Mamelodi Sundowns Football Club yatwaa ubingwa African Football League

PRETORIA-Dimba la Loftus Versfeld lililopo jijini Pretoria nchini Afrika Kusini limegeuka kuwa shubiri kwa Wydad Athletic Club ya Morocco.

Ni baada ta wenyeji Mamelodi Sundowns Football Club ya huko Mamelodi, Pretoria katika Jimbo la Gauteng kuwanyuka mabao 2-0 katika michuano ya African Football League.

Wenyeji hao ambao waliasisiwa mwaka 1970 waliutumia vema uwanja wao wa nyumbani ambao umewawezesha kutwaa taji hilo jipya kwa mara ya kwanza.

Peter Taanyanda Shalulile dakika ya 45+ na Aubrey Maphosa Modiba dakika ya 53 ndiyo waliwafanya waajiri wao hao kutwaa tai hilo ambalo limeambatana na kitita kikubwa cha fedha.

Aidha, Mamelodi Sundowns wanakuwa washindi wa kwanza wa African Football League ikiwa ni michuano inayoandaliwa kwa pamoja na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) kwa ushindi wa jumla wa 3-2.

Ni kufuatia kufungwa 2-1 kwenye mchezo wa kwanza Jumapili iliyopita mjini Casablanca nchini Morocco ambapo
kwa ushindi huo, Mamelodi Sundowns wanapata zawadi ya dola za Kimarekani milioni 4 (zaidi ya shilingi bilioni 9 za Kitanzania).

Kwa upande wao, Wydad Club Athletic inapata dola milioni 3 huku Al Ahly ya Misri na Esperance ya Tunisia zilizoishia nusu fainali kila moja inapata dola milioni 1.7.

Vile vile,TP Mazembe ya DRC, Enyimba ya Nigeria, Petro Atlético ya Angola na Simba ya Tanzania kila moja imepata dola milioni 1 kwa kushiriki michuano hiyo ya timu nane barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news