Rais Dkt.Mwinyi azungumza na Rais wa Romania na kumwandalia dhifa maalum


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na mgeni wake Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis, alipowasili Ikulu jijini Zanzibar kwa mazungumzo na kuandaliwa dhifa maalum iliyofanyika katika viwanja vya Zanzibar akiwa katika ziara yake ya siku moja Zanzibar tarehe 18 Novemba.(Picha na Ikulu).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Rais wa Romania, Mhe. Klaus Iohannis, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Zanzibar, na kujumuika katika dhifa maalum aliyomuandalia mgeni wake katika viwanja vya Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika picha ya pamoja wageni wake (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Romania, Mama Carmen Iohannis na Rais wa Romania, Mhe.Klaus Iohannis, baada ya kumaliza mazungumzo yao na dhifa maalum aliyowaandalia katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar wakati wa dhifa maalum aliyomuandalia mgeni wake Rais wa Romania Mhe. Klaus Iohannis,baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu, akiwa Zanzibar kwa ziara ya Siku moja.
Rais wa Romania Mhe.Klaus Iohannis akizungumza katika viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar wakati wa hafla ya dhifa Maalum aliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, iliyofanyika akiwa Zanzibar kwa ziara ya siku moja.

Rais mstaafu wa Zanzibar, Mhe.Ali Mohamed Shein na (kushoto kwake) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziba,r Mhe.Hemed Suleiman Abdullah, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar ,Mhe.Zuberi Ali Maulid na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt.Said Mohammed Dimwa, wakihudhuria dhifa maalum iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi, kwa mgeni wake Rais wa Romania Mhe.Klaus Iohannis, katika viwanja vya Ikulu, akiwa Zanzibar kwa ziara ya Siku Moja Zanzibar.

Viongozi wa Vyama vya Siasa Zanzibar wakihudhuria katika dhifa maalum iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa ajili ya mgeni wake Rais wa Romania Mhe.Klaus Iohannis, iliyofanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar, wakati wa ziara yake Zabzibar kwa siku moja.


Mabalozi Wadogo wanaofanyia kazi zao Zanzibar wakihudhuria katika dhifa maalum iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi katika viwanja vya Ikulu jijini Zanzibar , wakati wa ziara ya siku moja ya Rais wa Romania, Mhe.Klaus Iohannis Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news