Rais Dkt.Samia amkabidhi nyumba mjane wa Hayati Dkt.John Pombe Joseph Magufuli


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo 5 Novemba, 2023, akimkabidhi mfano wa ufunguo mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Mama Janeth Magufuli ikiwa ni ishara ya kukabidhi nyumba mpya ya kuishi kwa familia ya Dkt. John Pombe Magufuli iliyopo wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam ambayo amejengewa na Serikali kwa mujibu wa sheria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla fupi ya kukabidhi nyumba ya kuishi iliyopo wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023, ambayo imejengwa na Serikali kwa mujibu wa sheria,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa nyumba mpya ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, na kuikabidhi kwa Mama Janeth Magufuli, nyumba hiyo imejengwa na Serikali kwa mujibu wa sheria, Jijini Dar es Salaam tarehe 5 Novemba, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news