Serikali yaahidi kuwekeza zaidi katika kilimo nchini

DAR ES SALAAM-Kaibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya amesema kuwa, Serikali inafahamu umuhimu wa kilimo kwa uchumi wa nchi na kuutambua mchango wa TADB katika kutoa mikopo yenye riba nafuu kwenye kilimo, hivyo Serikali itaendeleo kuwekeza kwenye kilimo.

Mwandumbya ameyasema hayo wakati akizindua Mpango Mkakati wa Miaka Mitano (2023-2027) (Medium Term Strategy) wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).

Sambamba na bidhaa za kifedha za benki hiyo zinazolenga kuboresha kilimo hapa nchini, katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JINCC) jijini Dar es salaam.

“Mwaka 2022/23, Serikali imewekeza jumla ya shilingi 751.1 billioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 155.3% kutoka shilingi 294.16 billioni ilizowekeza katika sekta ya kilimo mwaka uliotangulia.

"Ongezeko hili kubwa linadhihirisha wazi nia ya Serikali kuleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya kilimo,”amesema.

Aidha, Bw. Mwandumbya ameupongeza uongozi wa benki hiyo pamoja na wafanyakazi kwa kukuza ufanisi wa benki kwa kuongeza wigo wa huduma zake, huku akiwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news