Watumishi 11 wafikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhujumu uchumi Manispaa ya Ujiji

*Ni matokeo ya kamati iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kubainika kuwepo kwa mtandao wa wizi

KIGOMA-Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora Athuman Msabila na wenzake 10 wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kigoma kujibu tuhuma za uhujumu uchumi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Akisoma mashtaka 11 yanayowakabili watuhumiwa hao, Wakili mwandamizi wa Serikali Anosisye Erasto amesema watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa pamoja katika kesi ya uhujumu uchumi namba tatu ya mwaka 2023 wakiwa wametenda makosa ya kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kughushi nyaraka, matumizi mabaya ya madaraka, kutakatisha fedha na kuisababishia Serikali hasara ya 463.5.

Wakili mwandamizi Anosisye amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji na baadae kuhamishiwa wilayani Igunga Athuman Msabila, Aidan Mponzi, Tumsifu Kachira na Ferdinand Filimbi,

Wengine ni Salum Said, Mosses Zahuye, Joel Shirima, Jema Mbilinyi, Kombe Kabichi, Frank Nguvumali na Bayaga Ntamasambilo wote wakiwa ni watumishi wa kada mbalimbali katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Ofisi ya Rais (TAMISEMI).
Wakili Mwandamizi wa Serikali Anosisye Erasto ameileza mahakama wakati kesi hiyo ikisomwa kwa mara ya kwanza kuwa watuhumiwa hao wanatuhumiwa kutenda makosa hayo kati ya Juni 01, 2022 na Juni 05, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news