Waziri Mhagama aagiza miundombinu ya mawasiliano iimarishwe Dar

DAR ES SALAAM-Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imeahidi kutoa shilingi milioni 20 ili kuimarisha kivuko cha Magole/Mwanagati kilichopo katika Kata ya Mzinga ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ilala mkoani Dar es salaam ili kiweze kupitika muda wote.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu), Mhe, Jenista Mhagama akiangalia uharibifu wa kivuko cha Magole/Mwanagati uliotokana na katika ziara yake Mkoani Dar es Salama iliyolenga kupata taarifa zilizochukuliwa na Kamati ya Mkoa ya Maafa juu ya kudhibiti madhara ya zaidi mvua yanayoweza kujitokeza.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.Jenista Mhagama wakati akizungumza na wakazi waliojitokeza katika eneo hilo la kivuko liloathirika na Mvua wakati wa ziara yake iliyolenga kupata taarifa zilizochukuliwa na Kamati ya Mkoa ya Maafa juu ya kudhibiti madhara ya zaidi mvua yanayoweza kujitokeza.

Ameongeza kusema kazi ya kuimarisha kivuko ifanywe na wakala wa barabara vijijini TARURA haraka iwezekanavyo.

“Kivuko hiki kitakapokuwa kinapitika muda wote hakitarudisha juhudi ya kwenda na Mpango wa pili wa muda mrefu wa kujenga daraja la kudumu,”alibainisha.
Waziri mhagama alisema kuwa serikali inatamani kuona shughuli za wananchi zifanyika bila kusimama; tunatamani watoto wetu waende shule, tunatamani kina mama wajawazito waende kupata huduma za afya kwa wakati, tunapenda wananchi wajisikie serikali yao inawajali, alisema Waziri.

“Tunataka tutengeneze daraja livutie machoni pa watu, kile matumaini kwa watu kwamba hii ni nyota ya Mhe. Rais, Dkt, Samia Suluhu Hassan na wananchi washirikishwe kiasi cha kutosha,” alifafanua

Waziri Mhagama alielekeza TARURA kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu mkubwa na kwa hofu ya mungu, kwa sababu mnasimamia uhai na maisha ya watu na sisi tunawaamini na tunawategemea.
Katika hatua nyingine Waziri ameomba wananchi kuendelea kuchukua tahadhari juu ya magonjwa ya mlipuko; hali ya mvua inaweza kutupelekea kwenye magonjwa ya kuhara, magonjwa ya malaria.

Aliwaasa wananchi kuendelea kusafisa vichaka na kujenga utaratibu mzuri wa kusafisha mazingira yetu na kila mmoja awe askari wa mwenzake na kuhakikisha mifereji yetu inakuwa safi na mapito ya maji yanakuwa wazi.

Kwa upande Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe. Albert Chalamila alisema, Mkoa wa Dar es salaam umeathiriwa na wa ujenzi wa kutawanyika, hivyo kasi ya ujenzi wa miundombinu imekuwa gharama kubwa, lakini lazima hilo lifanyike kwa sababu ni huduma kwa watanzania.

Wataalamu wetu wamekuwa wakisanifu ramani za daraja lakini bado hatujapata fungu la fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja, na hapa tunahitaji mkakakati mkubwa wa kuzuia mto kutokula kingo zake.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe, Jenista Mhagama na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila wakiangalia uharibifu wa barabara inayopita katika kivuko cha Magole/Mwanagati wakati wa ziara yake mkoani Dar es Salaam.

"Tunajitahidi kuhakikisha wananchi hawajengi mabondeni; na kulinda mito dhidi ya shughuli za kibinadamu, ikiwa ni sambamba na kuhakikisha tunaunganisha miundo mbinu ya mawasiliano ili mambo yaweze kwenda vizuri,” alifafanua Mkuu wa Mkoa.

Naye Diwani wa Kata ya Mzinga, Jackob Izack amesema, kero ni kubwa na kumshukuru sana waziri kwa kuja, mipango ilikwisha pangwa, mahitaji ya wananchi ni mikubwa na kuna wananchi zaidi ya elfu ishirini wanapita kila siku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news