Yanga kwa Simba SC huwa hawavuki mabao 5? miaka 65 Simba inajivunia mabao 6-0 tu

DAR ES SALAAM-Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salalam imerejea katika historia yake ya miaka 65 iliyopita baada ya kuwachakaza watani zao Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam mabao 5-0.

Ni baada ya Novemba 5, 2023 katika Dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kupitia michuano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kuwatembezea kichapo hicho ambacho kinafanana na kile cha Juni Mosi,1968.

Ikumbukwe kuwa, mtanange huo ulipigwa kipindi hicho ambacho Simba ikifahamika kama Sunderland ambapo magoli ya Yanga yalifungwa na Saleh Zimbwe,Maulid Dilunga na goli moja alifunga Kitwana Manara.

Vile vile katika mtanange wa Novemba 5, 2023 kikosi cha Yanga kilipata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa Kennedy Musonda kwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Yao Attohoula.

Kibu Denis aliwapatia Simba SC bao la kusawazisha kwa kichwa dakika ya tisa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Said Ntibazonkiza.

Max Nzengeli aliwapatia Yanga bao la pili dakika ya 64 kwa shuti kali la chini chini baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu wa Kati.

Aziz Ki aliwapatia Yanga bao la tatu dakika ya 72 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clement Mzize.

Nzengeli aliwapatia Yanga bao la nne dakika ya 77 akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi ya Mzize. Bao la tano kwa klabu ya Yanga lilipelekwa nyavuni na Pacome dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti.

Ingawa baada ya kipigo hicho cha kushitua,Julai 19,1977 wana Msimbazi walijiwekea rekodi yao ya kipekee kwa kuitandika Yanga mabao 6-0.

Magoli ya Kibadeni yalitinga nyavuni dakika ya 10, 42, na 89 huku Seleman Sanga akijifunga na Ezekiel Greyson akahitimisha. Ushindi huo ulidumu kwa miaka mingi.

Aidha, katika mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ambayo ilichezwa Mei 7, 2012 Yanga SC ilikataa kuburuzwa na kuwachapa mabao 5-0 Klabu ya Simba.

Ushindi huo uliotokana na mabao ya Emmanuel Okwi mawili dakika ya 2 na 62, Felix Sunzu kwa penalti dakika ya 56, Juma Kaseja kwa penalti dakika ya 67 na Patrick Mafisango (marehemu) kwa penalti dakika ya 72.

Mtanange wa Novemba 5, 2023 ni wa 111 kwa klabu hizo kukutana katika Ligi Kuu Bara ambapo Klabu ya Yanga imeshinda mitanange 39 ikatoka sare 40 huku ikifunga mabao 118 na kuruhusu 104 na Simba SC imeshinda mechi 32.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news