Baba yake Lengai Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM Mkoa wa Arusha

ARUSHA-Loy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Arusha.
Ushindi huo unakuja baada ya Chama Cha Mapinduzi kufanya Kikao cha Kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM hivi karibuni ambapo pamoja na mambo mengine, kikao hicho kilijadili hali ya Kisiasa ndani ya chama na nje ya chama.

Aidha, kilifanya uteuzi wa mwisho wa wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya chama kwa ngazi ya mkoa na wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali.

Kupitia uchaguzi huo uliofanyika Ukumbi wa AICC jijini Arusha,Loy Thomas Sabaya ameshinda kwa kupata kura 463 kati ya kura 907 zilizopigwa katika nafasi ya mwenyekiti.

Anthony Mtaka ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe ndiye alikuwa msimamizi wa Uchaguzi huo.

Huku Dkt.Daniel Mrisho Pallangyo akipata kura 374,Solomoni Olesendeka Kivuyo amepata kura 59,Edna Israel Kivuyo amepata kura 10 na kura moja ikaharibika.

Uchaguzi huo umefanyika baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha ndugu Zelothe Stephen kufariki dunia Oktoba 26,2023.

Zelothe alifariki alipokuwa jijini Dar es Salaam, alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

3 Comments

  1. ONGERA SANA WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM MKOA WA ARUSHA KWA UCHAGUZI SAFI NA KUMLETA MWENYEKITI MPYA WA CCM MZEE WETU LOY THOMAS OLE SABAYA

    ONGERA SANA WAJUMBE NA KONGOLLE KWA HUTUBA NZURI SANA TAKUTO KUTAKA KUKWAMISHANA KWENYE SAFU KAMA VIONGOZI KATINA UTENDAJI WA CHAMA NA SEREKALI YAKE NDANI YA MKOA WA ARUSHA

    KATIKA DHANA YAKUTO TAKA KUKWAMISHANA NATAKA NIWAPE SIRI KWANINI KURA MOJA ILIARIBIKA KWENYE UCHAGUZI WAZIWAZI IKO WAZI LIVE PLEASE

    NA KURA IYO SIO YA MWINGINE NI YULE YULE MKWAMISHAJI WA MKOA WA ARUSHA ALIO CHEKELEA KIFO CHA MWENYEKITI ZELOTE NA KWENYE UCHAGUZI MDOGO ALIWEKA WAGOMBEA WAKE 27 NA WOTE WALIKOSA SIFA NA MASHIKO KWENYE KAMATI KUU YA CCM TAIFA NA HALIMASHAURI KUU YA CCM TAIFA

    NA MKWAMISHAJI UYU SIO MWINGINE NI YULE MBUNGE MWENYE KIBURI ZARAU NA MAJIVUNO ASIO SHAURIKA KWENYE MKOA WA ARUSHA

    NAKWA ZARAU KUBWA SANA LEO BAADA YA KUONA KUWA AWEZI IFICHA ROHO YAKE MBAYA KWENYE CHAMA NA SEREKALI YA CCM AKIWA KWENYE UKUMBI ALIMWAMBIA MJUMBE MMOJA WAZI APA ATA NIKIJIPENDEKEZA SIWEZI PENDWA KILICHO BAKI MMI NAENDA KUARIBU KURA YANGU ILI TU ASIWE MNAFKI KWENYE MOYO WAKE

    NA NDIVYO ALIVYO FANYA KUARIBU KURA WAZI YANI ASIPIGE KOKOTE WALA KUANDIKA CHOCHOTE KWA SABABU KATIKA WAGOMBEA WOTE ALIKUWA HANA CHAGUO LAKE

    NA MJUMBE UYO MWENYE DHANA NA MIPANGO NA KAMASIO MIKAKATI YA KUKWAMISHANA NI MBUNGE WA ARUSHA JIJI MRISHO MASHAKA GAMBO

    SINA HATIA PAKA SASA MSIMAMO WANGU NI ULE ULE ARUSHA BILA GAMBO AKUNA KUKWAMISHANA MSIJE SEMA SIKUSEMA LIVE PLS

    ReplyDelete
  2. Kwa Mkoa Wa Arusha inahitaji Mwenyekiti Mkali kidogo Kwa Kuwa Mkoa huu Hususani Arusha Mjini Kuna Uhuni Mwingi Imani Yangu Wana Arusha wamechagua Fungu lililo Jema Nina Imani CCM Mkoa Wa Arusha itatulia.

    ReplyDelete
  3. Huyu alikuwa DC nyumbani kwetu Serengeti na ndipo sabaya Jr alipokulia na kusoma shule jirani ya ikizu sekondari

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news