Balozi Mwamweta awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani

BERLIN-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Mheshimiwa Hassan Iddi Mwamweta amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani, Mheshimiwa Frank Walter Steinmeier katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Berlin.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Hati hizo Mheshimiwa Rais Frank Walter Steinmeier alifafanua kuwa Serikali yake inaunga mkono jitihada za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais was Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tanzania na Ujerumani zinashirikiana kwenye maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa miradi ya afya; elimu; utunzaji wa mazingira; utamaduni; uhifadhi wa mazingira; utalii; biashara; uwekezaji pamoja na kubidhaisha kiswahili.
Itakumbukwa pia katika jitihada za kuimarisha ushirikiano Mheshimiwa Steinmeier alifanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania kuanzia tarehe 30 Oktoba mpaka tarehe 1 Novemba 2023 akiwa ameambatana na ujumbe wa Makampuni mbalimbali kwa ajili ya kuangalia fursa ili kuwekeza nchini.
Pamoja na ratiba nyingine akiwa nchini alifanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo mazungumzo ya viongozi hao yalijikita katika kuendeleza na kukuza ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kwa maslahi ya pande zote mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news