Kyela watakiwa kulima kilimo cha kakao kibiashara

MBEYA-Wananchi wa Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya wametakiwa kufanya kilimo biashara katika zao la kakao ili kuinua uchumi wao kutokana na zao hilo kuzidi kupanda bei.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exaud Kigahe (Mb) akiangalia tunda la zao la Kakao katika Shamba darasa la Bw. Isaya Wilayani Kyela Desemba 18, 2023.
Ushauri huo umetolewa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Exaud Kigahe(Mb) Desemba 18,2023 wakati wa ziara yake ya kuona maendeleo ya zao la biashara la kakao wilayani Kyela.
Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo amewataka Wizara ya Kilimo kupitia maafisa ugani kutoa elimu kwa wakulima ili kuzalisha kibiashara zaidi kwani zao hilo limekuwa na faida kubwa katika kuinua uchumi wao na Taifa kwa Ujumla.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Bw. Asangye Bangu na Mkuu wa Wilaya ya Kyela Mhe. Josephine Manase wakiangalia miti ya kakao katika shamba la Kakao la Bw. Isaya pamoja na kushiriki zoezi la mnada namba 25 wa Kakao wilayani hapo Desemba 18, 2023 katika ziara ya kikazi Wilayani Kylea yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi za Ghala katika zao la Kakao.

Aidha, Mhe Kigahe amezielekeza Taasisi za SIDO na TIRDO kufanya utafiti wa namna ya kuzalisha bidhaa ya ziada inayotokana na mbegu ya zao hiyo ikiwemo kuzalisha juisi na pombe ya kisasa.
Vilevile Mhe.Kigahe amesema kuwa ziara hiyo ina lengo la kuhakikisha Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji wa biashara katika kilimo hususani wa zao hilo pamoja na kufurahishwa na mfumo wa stakabadhi ghalani na kupanda kwa bei ya zao la Kakao kutoka Sh 9,800 mpaka Sh10,000.
Naye Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Josephine Manase amewataka wananchi na wakulima wa zao hilo wilayani hapo kulilimda zao la kakao pamoja na kuacha tabia ya kuuza zao hilo kwa watu wakati badala yake wafike katika minada inayotangazwa ili kuuza zao hilo kwa bei elekezi inayotolewa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala,Ndg.Asangye Bangu akizungumza na Wakulima wa Zao la Kakao Wilaya Kyela juu ya Umuhimu wa kuweka Zao la kakao yebye ubora kwenye ghala.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Stakabadhi za Ghala Ndg.Asangye Bangua amewataka wakulima kuhakikisha wanapeleka kakao kwenye maghala lakini pia kuhakikisha tunapeleka kakao yenye ubora kwenye ghala na kwa kufanya hivyo kutaongeza kujihakikishia soko la uhakika la kakao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news