Profesa James Shaba afariki

CHICAGO-Daktari bingwa wa utambuzi wa magonjwa na sababu za vifo, Profesa James Shaba amefariki dunia Desemba 5, 2023.
Profesa Shaba ndiye aliyefanya uchunguzi wa mwili wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Hayati Edward Sokoine, kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Sokoine alifariki Aprili 12, 1984 akiwa na umri wa miaka 45 kutokana na ajali ya gari iliyotokea Dakawa mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia ya Profesa Shaba inasema kuwa,baba yao alifariki majira ya saa mbili usiku, Chicago nchini Marekani alipokuwa akiishi.

Mtoto wa marehemu, Anale Shaba amesema taratibu za maandalizi ya mazishi zitatolewa baadaye na kwamba marehemu Shaba ameugua kwa muda mrefu.

Taarifa ya Familia
Wanajumuia,

Familia ya Professa James Shaba inasikitika kuwatangazia kuwa Mzee wetu Professa James Shaba amemaliza safari yake hapa duniani. Mzee wetu ametutoka jioni ya leo siku ya Jumanne tarehe 5 December 2023, muda wa saa 2:30 usiku saa za Marekani (Central Eastern Time) Chicago.

Habari zaidi za maandalizi ya mazishi zitatumwa baadaye. Mzee alikuwa akiuguzwa na watoto wake Stella na Anale Shaba kwa muda mrefu. Mungu aipumzishe roho ya mzee wetu mahali pema peponi.

Kwa mtakawatoweza kuawasiliana au kwenda kuwaona Stella na Anale Shaba (Watoto wa Marehemu) na Wana Chicago wenzetu mnaweza kusailiana nao kwa kupitia namba ya simu hapo chini au kwenda kuwaona nyumbani kwao:

Anale Shaba: (847) 525-9224
4151 N. Richmond
Chicago, IL 60618

“Bwana ametoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news