Prof.Janabi ateta na vyama vya wafanyakazi Upanga na Mloganzila

DAR ES SALAAM-Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof Mohamed Janabi leo amekutana na Viongozi wa Chama cha Wafanyakazi Madaktari na Wafamasia Tanzania (TMDPWU), Chama cha Wauguzi (TANA) na Chama cha Wafanyakazi wa Afya (TUGHE) na kujadili masuala mbalimbali yanayohusu uboreshaji huduma na maslahi ya wafanyakazi kwa ujumla wake.
Katika kikao hicho Prof. Janabi amewaasa viongozi wa vyama hivyo kufanya mikutano ya mara kwa mara na wanachama wao na kujibu hoja ambazo ziko ndani ya uwezo wao ikiwemo kusisitiza nidhamu ya kazi.
Amewashukuru kwa mshikamano wao na utulivu uliopo wakati wote mahali pa kazi na kuwaomba waendelee hivyo.
Kwa upande wao viongozi hao wameipongeza Menejimenti ya Hospitali kutokana na maboresho mbalimbali yaliyofanyika ya huduma na miundombinu na kuomba kuendelea kuboresha zaidi maslahi ya wafanyakazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news