Sasa ni New Amaan Sports Complex kutoka Amaan Stadium

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameridhia ushauri wa kuubadili jina uwanja wa Amaan na kuitwa New Amaan Sports Complex wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya Uwanja huo uliofanyika Desemba 27, 20203 kisiwani humo.

Rais Mwinyi ameridhia ushauri huo uliotolewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alipokua akitoa salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Kutokana na maboresho makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na kuufanya uwanja huu kuwa wa kisasa na wenye viwango vya Kimataifa, mimi naomba niubadilishe jina uitwe New Amaan Stadium." alisema Dkt. Ndumbaro.

Hafla ya Uzinduzi wa Uwanja huo ilipambwa na burudani mbalimbali ikiwemo Muziki na mechi ya mpira wa miguu ya kirafiki baina ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania Bara "Kilimanjaro Stars" na Timu ya Mpira wa Miguu ya Zanzibar "Zanzibar Heros ambazo zilitoka sare ya bila kufungana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news