TANROADS yarejesha mawasiliano Barabara ya Bagamoyo

NA GODFREY NNKO

WAKALA wa Barabara Tanzania (TANROADS) imerejesha mawasiliano ya barabara Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kupitia Bagamoyo.
Ni baada ya daraja la Mpiji linalounganisha mikoa hiyo kupata changamoto ya kumomonyoka kutokana na mvua za El-nino.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba 9, 2023 na Kitengo cha Uhusiano, Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, daraja hilo ambalo lipo mpakani mwa mikoa hiyo lilifungwa Desemba 8, 2023 kwa ajili ya usalama wa wasafiri.

Aidha, daraja hilo limefunguliwa Desemba 9, 2023 saa 12 asubuhi baada ya wataalam kufanya jitihada za kutengeneza hitilatu iliyojitokeza.

Vile vile, TANROADS imeruhusu watumiaji wa barabara hiyo kupitia upande mmoja wa daraja baada ya matengenezo kukamilika huku timu ya wataalam wa TANROADS wakiendelea kufanya matengenezo mengine ya haraka kulirejesha daraja hilo kwenye hali yake ya awali na kulifanya liwe na uimara zaidi.

“TANROADS inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza kuanzia Ijumaa tarehe 8 Desemba, 2023,”imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news