Wizara, wadau wa afya wajadiliana magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele

MOROGORO-Wizara ya Afya kupitia Idara ya Kinga Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani imefanya kikao cha wadau wa Afya Moja katika kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele kuanzia tarehe 13 Disemba Hadi tarehe 15 Disemba 2023 Mjini Morogoro.
Kikao kimekutanisha Wadau kutoka Wizara ya Afya na Wizara mtambuka na Taasisi kama vile (Ofisi ya Rais TAMISEMI, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Ofisi ya Waziri Mkuu, Maji, Kilimo, Mifugo, Elimu) Taasisi za Utafiti, Vyuo Vikuu, na Wadau wa Maendeleo

Kikao kililenga kufanya uchambuzi wa awali (situation analysis) wa mbinu ya Afya Moja katika kukabiliana na magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele hasa yale yanayoambukizwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

Akifungua Kikao hicho Dkt. Tumaini Haonga ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga amesema

"Tanzania inajivunia kuanzishwa kwa Kurugenzi Maalum ya Uratibu wa Afya Moja ndani ya Ofisi ya Waziri Mkuu, yenye lengo la kuoanisha afua katika Wizara zote ili kudhibiti Magonjwa yanayohitaji ushirikishwaji wa Sekta mbalimbali.

Zaidi ya hayo, amesema Mpango Jumuishi wa Kitaifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele (NTDCP), ulianzishwa mwaka 2009 chini ya Wizara ya Afya ili kuweza kuratibu Magonjwa haya.

Hata hivyo, licha ya juhudi hizi zilizoratibiwa, bado Magonjwa ya NTDs hasa yanayoambukizwa kutoka wanyama kwenda kwa binadamu yanaendelea kupokea uangalizi duni kutoka kwa mifumo ya huduma za afya, taasisi za utafiti, Elimu na watunga Sera"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news