Yajayo Zanzibar yanafurahisha,Rais Dkt.Mwinyi akabidhiwa ramani mji mpya wa kisasa

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekabidhiwa mfano wa ramani ya Mji mpya wa biashara na uwekezaji, Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B Mkoa wa Mjini Magharibi.
Rais Dkt. Mwinyi akipokea ramani hiyo Ikulu, Zanzibar kutoka kwa Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Mhe. Omar Said Shaaban, amepongeza hatua za awali zilizofikiwa na wazo la ujenzi wa Mji huo.
Naye Waziri Shaaban alisema ujenzi wa Mji huo wa kisasa utajumuisha ikiwemo ukumbi mkubwa wa mikutano wa kisasa wa kimataifa, Hoteli kubwa za kisasa zenye hadhi ya nyota tano, ujenzi wa eneo la kisasa la biashara litakalohusisha maduka makubwa, Makaazi ya kisasa ya Wananchi, ujenzi wa Hospitali ya kisasa pamoja na kuwekwa viwanja vya Michezo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news