Rais Dkt.Mwinyi:Tumedhamiria kuimarisha Sekta ya Michezo

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema, Serikali ya Zanzibar itaendelea kuweka mazingira bora ya michezo ili kuimarisha vipaji vya wanamichezo.
Mhe. Mwinyi ametoa kauli hiyo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi, la ukarabati wa Uwanja wa Amaan Studium pamoja na ujenzi mpya wa miundombinu ya uwanja huo.

Amesema azma ya Serikali ni kuimarisha sekta ya Michezo kwa kuendeleza na kuibua vipaji vya wanamichezo ili kuleta maendeleo Nchini.

"Sasa hivi hatuna shaka vipaji tunavyo vya michezo mbalimbali tunachohitaji mazingira bora,"alisema Dkt.Mwinyi.

Aidha, alieleza kuwa uwanja huo utatumika kwa michezo ya aina mbali mbali ikiwemo Mpira wa miguu, Judo, Mpira wa kikapu, Mpira wa wavu, mpira wa mkono, na mengineyo.

Dkt. Mwinyi ameipongeza Kampuni ya Orkun ya Uturuki kwa juhudi waliyoifanya ya kukamilisha ujenzi wa Uwanja huo kwa wakati na kwa kiwango cha kimataifa.

Naye Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe, Tabia Maulid Mwita amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi Kwa jitihada zake kubwa katika kusimamia michezo nchini.

Aidha, Waziri Tabia amesema Uwanja huo unakila sifa na vigezo vya kuitwa Amaan Sports Complex hivyo amemuomba Rais wa Zanzibar kulitumia jina hilo badala ya Amaan Studium.

Uwanja wa Amaan Stadium unatarajiwa kuzinduliwa Rasmin hivi karibuni katika Shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar na kutumika katika michuano ya kombe la Mapinduzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news