Young Africans SC lazima tuifunge Medeama SC-Miguel Gamondi

KUMASI-Kocha Mkuu wa Yanga SC,Miguel Gamondi amesema, lazima washinde mtanange wao dhidi ya wenyeji Medeama ya Ghana.

"Lazima tushinde mechi yetu ya kesho mbele ya Medeama ili tufuzu hatua inayofuata, najua sio rahisi ila tutaweza kesho kupata alama, tumepata alama moja kwenye kundi ila timu yetu imefanya vizuri kwenye michezo iliyopita.

“Leo ndio nitajua kwenye maandalizi yetu ya mwisho nini nitaenda kufanya ila alama tatu za kesho ni lazima kwa sababu ni muhimu kwetu.

"Tunajua kundi letu ni gumu maana lina CR Belouizdad na Al Ahly timu ambazo zina uzoefu mkubwa wa mashindano haya ya CAF Champions League, wana uwezo mkubwa wana kila kitu na uzoefu wao sio wa kulinganisha na sisi.

"Ila niwaambie tu tunaanza hapa Medeama SC kusaka alama tatu pamoja na michezo yetu ijayo ya kundi hili na imani yangu inaniambia tutafuzu katikati yao CR Belouizdad na Al Ahly,"amesema.

Aidha, kikosi kimefanya mazoezi ya mwisho kuuzoea Uwanja wa Baba Yara jijini Kumasi nchini Ghana tayari kwa mchezo wake wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama.

Mtanange huo utapigwa Desemba 8, 2023 majira ya saa 1:00 usiku ambapo katika mechi zake mbili za mwanzo, Yanga SC ilifungwa 3-0 CR Belouizdad siku ya Novemba 24 uwanja wa Julai 5, 1962 jijini Algiers.

Vile vile walitoka sare ya 1-1 na mabingwa watetezi, Al Ahly Desemba 2,mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Aidha, Medeama mechi ya kwanza walichapwa 3-0 na Al Ahly tarehe 25 Novemba, 2023 jijini Cairo, kabla ya kushinda 2-1 nyumbani dhidi ya CR Belouizdad Desemba Mosi, mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news