Nje Sports yaigaragaza timu ya Ikulu Zanzibar mabao 8-3

ZANZIBAR-Timu ya Mpira wa Miguu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Nje Sports Football) imeigaragaza timu ya mpira wa miguu kutoka Ofisi ya Rais Ikulu Zanzibar magoli 8-3 katika mchezo ulichezwa uwanja wa Mao zedong’s Unguja, Zanzibar.
Nje Sports iliutawala mpira kwa asilimia kubwa ambapo kipindi cha kwanza iliongoza kwa magoli 5-1. Magoli ya nje sports yalifungwa na Ramadhani Chambuso (1), Said Kasanga (2), Selemani Mkonde (2), Fabian David (1) pamoja na Yakubu Kibiga (1).

Magoli ya timu kutoka Ofisi ya Rais Zanzibar yalifungwa na Khamis Ramadhan (1) pamoja na Seif Hatibu Ally (2).
Ushindi wa Nje Sports umeiwezesha kusonga mbele ambapo tarehe 11 Januari 2024 itacheza na Hazina katika uwanja wa Mao zedong’s Unguja, Zanzibar majira ya saa 16:00 kwa saa za Afrika Mashariki.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa timu ya Nje Sports, Shaban Maganga amesema kuwa lengo la timu yake ni kuimarisha kikosi na kujihakikishia ushindi katika michezo inayaofuata.

Kadhalika kocha huyo ameushukuru uongozi wa Wizara kwa kuwawezesha vyema hadi kufikia hatua hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news