Prof.Muhongo asema taarifa za Shule ya Msingi Wanyere B si sahihi

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara Prof. Sospeter Muhongo amesema picha iliyoko mtandaoni ikihusisha madai ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Wanyere 'B' iliyopo Kata ya Suguti Wilayani Musoma kusomea chini ya mti kutokana na upungufu wa vyumba vya madarasa siyo sahihi.
Prof. Muhongo ameyasema hayo Januari 9, 2024 kupitia taarifa yake ambapo amebainisha ukweli kuhusiana na shule za msingi Wanyewe.
"Nimeletewa picha hiyo iliyoko mitandaoni ikisemekana ni ya S/M Wanyere B, Kijiji cha Wanyere, Kata ya Suguti, Musoma Vijijini nimeongea na Headteacher kupata ukweli:

1. Picha hiyo siyo ya mazingira ya eneo la S/M Wanyere B.

2. Sura ya Mwalimu huyo ni ngeni haipo S/M Wanyere B.

3. Idadi ya wanafunzi iliyotajwa siyo ya S/M Wanyere B.

"Musoma Vijijini tunakiri, kama ilivyo sehemu nyingine nchini mwetu ya upungufu wa vyumba vya madarasa, na misongamano ya wanafunzi madarasani.

"Sisi (Musoma Vijijini) tunajenga, tukishirikiana na Serikali ya CCM, kutatua tatizo hilo ambalo chanzo chake kikuu ni ongezeko la idadi ya watanzania, wakiwemo watoto wadogo, kwa kasi kubwa!."

Mwaka 2006 - 2020:(Madarasa mapya 380)

Musoma Vijijini, tukishirikiana na Serikali yetu, tulijenga VYUMBA VIPYA vya Madarasa 380 kwenye Shule zetu za Msingi 111.

Mwaka 2006 - 2020 :(Madarasa mapya 120)

Musoma Vijijini, tukishirikiana na Serikali yetu, tulijenga Vyumba vipya vya Madarasa 120 kwenye Shule zetu za Sekondari 20.

Tokea Mwaka 2020 hadi leo hii, tunaendelea kujenga shule shikizi mpya, sekondari mpya, vyumba vipya vya madarasa, maabara mpya, maktaba mpya, n.k.

USHAURI WA PROF. MUHONGO.

"Mtoa habari mitandaoni, zisokuwa na uhakika, anashauriwa atembelee S/M Wanyere B na Musoma Vijijini kwa ujumla wake, kupata ukweli, na ajionee ujenzi na uboreshaji wa miundombinu ya elimu vijijini mwetu,"amefafanua Prof.Sospeter Muhongo (Mb).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news