Serikali yawekeza zaidi Muhimbili

DAR ES SALAAM-Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya hususani katika huduma za mama na mtoto kwa lengo la kupunguza vifo vitokananavyo na uzazi na kuhakikisha kuwa kila mtanzania anayezaliwa anakuwa salama.
Hayo yamesema na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo alipokuwa akiongoza zoezi la kufanya usafi na kupanda miti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ikiwa ni kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Rais Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mhe.Mpogolo ameeleza kuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kimbilio kwa kila mtanzania na kwa kutambua hilo Rais. Mhe. Dkt. Samia amewekeza vifaa tiba vya ambavyo vitaweza kumsaidia mama na mtoto anayekuja Muhimbili kupata huduma.
“Kwa kutambua umuhimu wa afya ya watanzania Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewekeza vifaa tiba hapa vya ttakribani shilingi bilioni 11, pia amechangia fedha zake binafsi kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuboresha huduma ya mama na mtoto na haya yote amefanya kwa dhati kabisa ili kumlinda mama na mtoto anayezaliwa,” amefafanua Mhe. Mpogolo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amewataka watanzania kutumia kutumia uwekezeji huo uliofanywa na Serikali katika kufanya uchunguzi wa afya zao kabla ya kuugua.
“Gharama za matibabu ni ghali hivyo ni vyema mkajenga tabia ya kufanya uchunguzi wa afya kwa kuwa kinga ni bora kuliko tiba, njooni mfanye uchunguzi wa afya zenu,”amesema Prof. Janabi.

Vilevile amewasisitiza wananchi kujitokeza kufanya uchunguzi wa saratani ikiwemo saratani ya matiti na mlango wa kizazi kwa wanawake na saratani ya tezi dume kwa wanaume kwa kuwa saratani ikigundulika mapema inaweza kutibika na mtu akapona kabisa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news