Simba SC kukusanya shilingi bilioni 25.94

DAR ES SALAAM-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam inatarajia kukusanya shilingi bilioni 25.94 katika bajeti yake mwaka 2023/24.
Hayo yamesemwa leo Januari 21, 2024 na Mhasibu wa klabu, Suleiman Kahumbu katika Mkutano Mkuu wa Klabu ya Simba 2023 ambao unafanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

"Matumizi ya 2022/23 yalipangwa kuwa shilingi 12,363,626,983 lakini matumizi halisi ni shilingi 15,936,829,943.

"Bajeti kwa mwaka 2023/2024 klabu imepanga kukusanya kiasi cha shilingi 25,930,722,300 lakini imepanga kutumia kiasi cha shilingi 25,423,997,354.

"Tutabaki na mapato ya ziada ya shilingi 506,724,946,"amebainisha Mhasibu wa Klabu, Suleiman Kahumbu katika mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news