Tume ya Tehama yawakutanisha wabunifu chipukizi kuongezewa ujuzi

DAR ES SALAAM-Tume ya Tehama nchini (ICTC) kupitia Programu ya Dunia Yetu imewakutanisha wabunifu chipukizi wa Tehama Mkoa wa Dar es Salaam na kampuni kubwa zilizofanikiwa katika sekta hiyo ili kuwapa fursa ya kuongeza ujuzi zaidi katika mifumo bora.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Tehama (ICTC), Dkt. Nkundwe Mwasaga amefafanua kuwa,tukio hilo wameliandaa kwa kushirikiana na Kampuni ya ThreeFold ikiwemo HoloChain.

"Sisi tunafanya kazi na kampuni za watu binafsi na vile vile watu wa nje, kwa hiyo tumempata Arthur Brock ambaye ana kampuni ambayo inajulikana Dunia nzima, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa, atazungumza na vijana wetu na atawapa siri za kutengeneza mifumo ambayo inaweza kuuzika duniani kote."

Aidha, Dkt.Mwasaga amefurahi kuona mwitikio mkubwa wa vijana ambao wameshiriki katika tukio hilo huku wakionesha utayari wa kujifunza kwa watu wengine. Tazama video chini kwa taarifa zaidi;
"Vijana wetu wako tayari, wako tayari kujifunza kwa watu ambao wako juu na hawa wenzetu nilijaribu kuwauliza kuhusiana na vijana wetu wakasema wana uwezo mkubwa.

"Kinachotakiwa tu ni kuwapa mbinu chache ili waweze kutengeneza vitu ambavyo vitaongeza nguvu yetu ya kupambana katika mambo ya Tehama duniani,"amefafanua Dkt.Mwasaga.

Aidha, tukio hilo la kuwaongezea ujuzi lilikuwa la kipekee kutokana na uwepo wa Arthur Brock akiwa ni mwasisi wa Kampuni ya HoloChain. 
Brock ni miongoni mwa wabobezi wa Tehama waliofanikiwa zaidi, ni ambao wanatajwa katika tano bora ya watu waliofanikiwa zaidi duniani.





Mbobezi huyo ambaye ni nadra sana kumpata kutokana na aina ya majukumu yake, ameonesha kuridhishwa na uelewa na utayari wa wabunifu chipukizi wa Kitanzania katika kujifunza na kuongeza maarifa, hivyo ameahidi kufanya kila linalowezekana kusaidia vijana wa Tanzania ili waweze kusonga mbele kupitia Tehama.

About the ICTC

The Information and Communication Technologies Commission (ICTC) was established by the Presidential Decree Government Notice (GN) No.532 published in the Government Gazette No. 4 Vol. 96 dated 20 November 2015.

 The ICT Commission provides the following functions in the area of ICT Promotion:

  • Promote ICT Professionals.
  • Promote Startups and Micro and Small and Medium Enterprises (MSME): Startups and SMEs are the backbones of the global economy. Globally they account for 50% of employment ad 90% of businesses.
  • Promote Regions in the digital economy(e.g. Dar es Salaam as ICT Driver and Engine of Growth).
  • Promote Tanzania to be competitive in the Digital Economy.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news