Waachishwa shule kwa madai Yesu anakaribia kuja kuwachukua

RUVUMA-Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma,Mheshimiwa Ngollo Malenya amefanya msako wa wanafunzi ambao hawajaripoti shule za nsingi na sekondari vijijini.
Katika hali isiyo ya kawaida alipofika Kijiji cha Chengena kwenye msako wa nyumba kwa nyumba amebaini uwepo wa mtumishi wa mungu Erick Manyanya (33) wa Kanisa la Country Living ambaye amefungua kanisa kijijini hapo akiwahubira wazazi wasiwapeleke watoto shule kwa kuwa Yesu Kristo atarudi muda sio mrefu, kuchukua kondoo wake hivyo badala ya kwenda shule wajiandae kumpokea Yesu.

Erick ni kijana ambaye alikuwa anasoma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye anadai baada ya kusoma vitabu na kuijua imani yake vizuri aliacha chuo na kwenda kuanzisha kanisa hilo Namtumbo.

“Nimesoma UDOM sikuhitimu elimu yangu sababu ni baada ya kuijua imani yangu vizuri katika vitabu, maana tumeambiwa mtu hatoishi kwa mkate tu bali kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu.

"Mpaka nafika Chuo Kikuu nipo katika mikono ya wazazi baada ya kujitambua mimi nachagua njia yangu inayonipa furaha, nyakati zinazokuja chapa ya mnyama itasurutishwa, kitabu cha ufunuo wa Yohana kuna namba 666 sasa huo wakati upo karibu yetu,”amedai.

DC Ngollo amesema Erick amefanikiwa kuwarubuni wazazi mbalimbali ambao ni wa dhehebu la Wasabato kijijini hapo na wameachisha watoto wao shule ili wajiandae kumpokea Yesu.

Amesema, hadi sasa watoto 13 tayari wameacha kwenda shule na wameaminishwa kuwa elimu ya Mungu haipaswi kuchangamana na elimu ya Dunia inayotolewa na shule za Serikali na binafsi.

Watoto wa Wasabato walioacha shule na kujiunga na kanisa hilo pamoja na wazazi wao ili kumsubiri Yesu ni pamoja na Abigaili Anthony Mkomela (13), Rachel Antony Mkomela (9), Setianthony Slavio (2).

Nathaniel Slavio (9), Irene Antony (18), Huria Antony Mkomela (6), Thabiti Mkomela ( 6), Seth Mkomela 6), Methew Makiluli ( 6), Lomanous Ngonyani (8), Sila Ngonyani (3), Bions Alfred (5), Lackson Alfred (8).

Mheshimiwa Ngollo akiwa na Kamati ya Usalama wa Wilaya ameagiza kukamatwa kwa Mwinjilisiti Erick na mwenzake anayemsaidia kazi za kanisa Anthony Mkomela.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news