Wakopaji wazidi kuonesha nidhamu, mikopo chechefu yapungua

NA GODFREY NNKO

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imesema kuwa,viwango vya mikopo chechefu vimepungua kutoka asilimia 5.8 iliyokuwepo mwaka juzi mpaka asilimia 4.3 iliyokuwepo Desemba mwaka 2023 nchini.
Hayo yamebainishwa leo Januari 19,2024 jijini Dar es Salaam na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba baada ya kutangaza kuanza rasmi kwa utekelezaji wa Sera ya Fedha kwa kutumia Mfumo wa Riba ya Benki Kuu “Central Bank Rate”.

Utekelezaji huo umeanza rasmi leo, hivyo kuachana na mfumo uliokuwepo wa Ujazi wa Fedha.

"Hiyo inaonesha pia kwamba, nidhamu ya wakopaji kurejesha mikopo imeongezeka na vihatarishi kwenye uhalisia wa kuchukua mikopo, kufanya biashara na mpaka kurejesha vimepungua.

"Na hali ya nidhamu ya matumizi ya fedha kuelekeza kwenye makusudio ya mikopo imeendelea kuongezeka.

"Kwa hiyo, ni wito wangu kwa Watanzania, yeyote anayehitaji kufanya biashara sasa hivi hali ya uchumi imeendelea kuimarika anaweza kupata fedha hizo kutoka kwenye mabenki kwa viwango vitajavyokuwa stahimilivu.

"Kwa sababu kiwango cha vihatarishi vya mkopaji kadri vinavyopungua ndivyo kile kiwango cha ukopeshaji kinavyoendelea kuongezeka.

"Kwa hiyo niendelee kuwahimiza Watanzania wenzangu kila anayechukua mkopo auchukue kwa makusudio sahihi.

Anapofanya biashara yake kwa kuwa uchumi umeendelea kuimarika afanye biashara yake vizuri.

"Arejeshe mkopo kwa wakati ili sisi tunaosimamia sekta hii ya fedha tuendelee kupunguza zaidi mikopo chechefu na hiyo itatusaidia viwango vya riba vitaendelea kupungua katika uchumi,"amefafanua Gavana Tutuba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news