Waziri Dkt.Ndumbaro afanya uteuzi Kamati ya Hamasa timu za Taifa

DAR ES SALAAM-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro ameteua Kamati Maalum kwa ajili ya hamasa kwa timu za Taifa zilizofuzu mashindano mbalimbali ya Kimataifa ambayo inaundwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu pamoja na Wajumbe 15.
Kamati hii itakuwa na jukumu la kuhamasisha Mashabiki na Wapenzi wa michezo ndani na nje ya nchi kujitokeza kuzishangilia na kuziunga mkono timu za Taifa pamoja na kuratibu hafla maalum ya harambee ya kuzichangia Timu za Taifa inayotarajiwa kufanyika Januari 10, 2024 jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa atamuwakilisha Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika hafla ya harambee hiyo.

Wajumbe wa Kamati walioteuliwa ni Theobald Sabi (Mwenyekiti), Patric Kahemela (Makamu Mwenyekiti) na Neema Msitha (Katibu) huku Wajumbe walioteuliwa wakiwa ni Beatrice Singano, Michael Nchimbi, Jemedari Said, Nick Reynolds (Bongo Zozo), Hamis Ali, Christina Mosha (Seven) , Mhandisi Hersi Said, Salum Abdallah (Try Again), Paulo Makanza – Mjumbe.
Wajumbe wengine ni Mohamed Soloka, Hassan Mohamed Raza, Lucas Mhavile (Joti), Oscar Oscar (Mzee wa Kaliua), Prisca Kishamba, Burton Mwemba (Mwijaku) na Clayton Revocatus Chipondo (Baba Levo).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news