ZIPA yapewa kongole uwekezaji

ZANZIBAR-Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe.Ibrahim Makungu imeipongeza Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA).
Ni kwa kufikia malengo ya uwekezaji ambayo yameiingizia Serikali fedha za kigeni zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 300 kwa kipindi cha muda mfupi.

Mhe. Ibrahim amesema,mabadiliko katika Sekta ya Uwekezaji ambayo yametokana na uwepo wa amani ya nchi na usimamizi wa Sera na Sheria ya Uwekezaji inayomfanya mwekezaji kuwekeza fedha zake nchini.
Aidha, Kamati hiyo imesema wakati umefika kwa ZIPA kuangalia uwezekano zaidi wa kukodisha visiwa vilivyobaki.

Lengo likiwa ni kupanua wigo wa utalii wa hali ya juu ambao kwa sasa umeshika hatamu duniani kote.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA, Shariff Ali Shariff amesema, kwa sasa ZIPA imejiwekeza sana kwenye mambo ya kimtandao kwa lengo la kurahisisha masuala ya uwekezaji na mwekezaji aweze kuomba uwekezaji popote alipo duniani.

Kikao hicho kimewashirikisha Kamati ya Utalii, Biashara na Kilimo ya Baraza la Wawakilishi na baadhi ya watendaji kutoka Wizara ya Nchi, Afisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news