Ajira kaa la moto nchi 10 za Afrika

NA DIRAMAKINI

MARA nyingi kupata ajira barani Afrika inaweza kuwa vigumu. Kwani, hakuna fursa za kutosha,licha ya kuzungukwa na rasilimali nyingi zenye kuchochea shughuli za uwekezaji na kuleta maendeleo.
Picha na WT.

Uchumi wa nchi nyingi za Kiafrika unaosuasua,hivyo unafanya fursa kuwa ngumu zaidi.

Licha ya kutekelezwa kwa mipango kadhaa ya serikali za Afrika ili kukabiliana na suala hilo, athari zake zimekuwa ndogo huku kukiwa na idadi kubwa ya watu wanaochechemea kiuchumi.

Ukubwa wa tatizo hilo uliwafanya viongozi wa Afrika kupitisha azimio lenye vipengele saba mwaka jana jijini Dar es Salaam ili kukabiliana na ukosefu wa ajira.

Barani Afrika, kama kwingineko duniani, idadi ya vijana iko katika hatari kubwa ya ukosefu wa ajira katika maeneo mengi duniani.

Kwa mujibu wa Statica, mwaka huu wa 2024, kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana barani Afrika kinakadiriwa kuwa karibu asilimia 11.

Pia, wanaume wanaona ni rahisi kupata kazi ikilinganishwa na wanawake, licha ya kuwa na ujuzi na uzoefu sawa.

Barani Afrika, kiwango cha ukosefu wa ajira kwa wanawake kilikuwa asilimia nane mwaka 2023, wakati kilikuwa asilimia 6.6 kati ya wanaume.

Aidha,tatizo la ukosefu wa ajira barani Afrika linakumba uchumi mkubwa na mdogo.

Kufikia leo, Afrika Kusini imefikia kiwango cha ukosefu wa ajira cha asilimia 32.1, na kuifanya kuwa nchi yenye kiwango cha juu zaidi cha ukosefu wa ajira katika bara la Afrika mwaka 2024.

Djibouti na Eswatini zinafuata kwa karibu, huku viwango vya ukosefu wa ajira vikifikia takribani asilimia 28 na asilimia 25 mtawalia.

Zifuatazo ni nchi 10 za Kiafrika zilizo na kiwango cha juu zaidi cha ukosefu wa ajira katika 2024:
RankCountryUnemployment rate
1South Africa32.1%
2Djibouti27.9%
3Eswatini24.65%
4Gabon21.35%
5Congo21.3%
6Botswana20.72%
7Somalia20.53%
8Namibia20.37%
9Libya20.07%
10Sudan18.05%

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news