Gauti ni nini?

𝐆𝐀𝐔𝐓𝐈 ni aina ya ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya Urea (uric acid) katika damu.
Ongezeko la uric acid husababisha madhara katika jointi (joint) (joint ni sehemu ya mwili inapokutana/ inapoungana mifupa miwili). Gauti inaweza kutokea ghafla (acute gout) au ikawa sugu (chronic gout). 

Gauti inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri jointi moja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri jointi zaidi ya moja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye jointi.

𝐕𝐈𝐒𝐀𝐁𝐀𝐁𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐕𝐘𝐀 𝐆𝐀𝐔𝐓𝐈.

Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha uric acid katika damu. Hali hutokea iwapo mwili wa mgonjwa unatengeneza uric acid nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa uric acid mwilini kama inavyotakiwa.

Ongezeko hili husababisha mrundikano wa uric acid katika maji maji yanayozunguka jointi yanayoitwa synovial fluid na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogo vidogo vya tindikali ya urea yaani uric acid crystals ambavyo husababisha jointi kuvimba na hatimaye kuathirika.

𝐕𝐈𝐇𝐀𝐓𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐈 (𝐫𝐢𝐬𝐤 𝐟𝐚𝐜𝐭𝐨𝐫𝐬).

Ingawa chanzo hakieleweki vema, ugonjwa wa gauti hutokea kuwapata baadhi ya watu walio katika familia moja. 

Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi kuliko wale wanaoendelea kupata hedhi.

Aidha,unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uric acid katika damu.

Vihatarishi vingine vya gauti ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo, unene uliopitiliza, ugonjwa wa sickle cell anemia au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).

Hali kadhalika, gauti inaweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo utendaji wake kazi huingiliana na utoaji wa uric acid mwilini.

𝐃𝐀𝐋𝐈𝐋𝐈 𝐙𝐀 𝐆𝐀𝐔𝐓𝐈

Kwa kawaida uhusisha jointi moja au joint chache. Jointi zinazoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa ha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.

Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla hususani nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.

Jointi hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). 

Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye jointi yenye matatizo.

Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, lakini pia laweza kujirudia mara kwa mara.

Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa

Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika jointi (chronic arthritis) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia jointi zake.

Wagonjwa wenye gauti kwa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka jointi zilizoathirika. 

Vinundu hivi kwa kitaalamu huitwa trophy na ni ishara ya muhimu kwa madaktari.

𝐕𝐢𝐩𝐢𝐦𝐨 𝐯𝐲𝐚 𝐠𝐚𝐮𝐭𝐢 𝐡𝐮𝐣𝐮𝐦𝐮𝐢𝐬𝐡𝐚.

Kiwango cha uric acid katika damu. Hata hivyo, si kila aliye na kiwango kikubwa cha uric acid katika damu huwa na gauti.

Kiwango cha uric acid katika mkojo

Uchunguzi wa maji maji yanayozunguka jointi (synovial fluid) kuchunguza vijiwe katika jointi
X ray ya jointi iliyoathirika
Uchunguzi wa utando unaozunguka jointi.

𝐏𝐚𝐭𝐚 𝐭𝐢𝐛𝐚𝐥𝐢𝐬𝐡𝐞 𝐢𝐬𝐢𝐲𝐨 𝐧𝐚 𝐤𝐞𝐦𝐢𝐤𝐨 𝐰𝐚𝐥𝐚 𝐦𝐚𝐝𝐡𝐫𝐚 𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐭𝐢𝐛𝐮 𝐯𝐲𝐚𝐧𝐳𝐨 𝐯𝐲𝐚 𝐭𝐚𝐭𝐢𝐳𝐨 𝐧𝐚 𝐤𝐮𝐩𝐨𝐧𝐚 𝐤𝐚𝐛𝐢𝐬𝐚.

𝐏𝐢𝐠𝐚 𝐚𝐮 𝐰𝐡𝐚𝐭𝐬𝐀𝐩𝐩
𝟎𝟕𝟔𝟔𝟎𝟑𝟏𝟒𝟕𝟎
𝟎𝟕𝟏𝟔𝟖𝟎𝟕𝟎𝟐𝟑

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news