Mwandishi Kazimbaya Makwega Adeladius asafirishwa toka Mwanza kwenda Dodoma

MWANZA-Ndugu waaandishi wenzangu muda huu nimefika Kituo Kikuu cha Polisi Kati na mawakili wa wawili wa OJADACT kufuatilia kukamatwa kwa mwandishi wa habari Kazimbaya Makwega Adeladius.
Kwa bahati nzuri tumemkuta hapa kituoni na nimepata nafasi ya kuongea naye ana kwa ana kama dakika tano hivi.

Wakati naongea naye wakaja maafisa waliojitambulisha kuwa wanatoka ofisi ya RCO Dodoma na wamekuja kumchukua ili waondoke naye.

Nao pia walikubali kuongea na mimi pia na sio mawakili nami nikafanya, hivyo tukaongea na wakaniambia wanaondoka naye kwenda Dodoma saa saba mchana.

Pia wakasema kuna tuhuma huko Dodoma za kujibu, hivyo tuwe na amani, kwani hizo ni tuhuma.

Hapo nikawauliza kuwa, kama wanatoka Dodoma mbona tumeongea na ofisi ya RPC Dodoma na ikathibitisha kuwa hakuna askari wake waliokuja Mwanza.

Wao wakajibu kuwa ofisi ya RPC ni kubwa ila wao wanatoka ofisi ya RCO Dodoma.

Maelezo toka kwa Makwega mwenyewe ni kuwa alikamatwa jana kwao Malya na akanyang'anywa laptop na simu zake tatu na pia alipofika hapa kituoni akaandikishwa maelezo.

Gari yenye namba za usajili SU 45605 LandCruiser imeondoka na Makwega hapa kituo cha polisi kati Mwanza.

Maelezo ya mwisho toka kwa watu wanaomshikilia walisema wataondoka saa saba mchana ila kwa sasa wanaenda wapi? Hatujajua na ilikuwa ngumu kuhoji.

Afya ya Makwega

Ipo salama kabisa, nilipoomba tumpe kwanza chai anywe wakasema watampa wao na hiyo ni haki yake kama binadamu hivyo watamhudumia.

Naomba wemzetu mlioko Dodoma jipangeni kwa ajili ya kumpokea.

Ushirikiano na Jeshi la Polisi

Tangu nilipofika kituoni nimepata ushirikiano mzuri na nilipojitambulisha wakamruhusu niongee naye kwa kina.

Ahsanteni sana wote

Edwin Soko
Mwenyekiti
OJADACT
MPC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news