Simba SC yaisogelea Yanga SC kileleni

DAR ES SALAAM-Simba SC imeibuka na ushindi wa bao moja katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa Uwanja wa Meja Jenerali Michael Isamuhyo.
Mchezo ulianza kwa kasi huku wakishambuliana kwa zamu na kutengeneza nafasi, lakini Simba SC walishindwa kuzitumia.

Clatous Chama aliwapatia bao la kwanza dakika ya 34 kwa shuti kali la nje ya 18 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Saido Ntibazonkiza.

Kipindi cha pili walionekana kuongeza kasi ya mashambulizi, lakini hata hivyo walishindwa kuyatumia.

Mzunguko wa kwanza wa Ligi umemalizika, Simba SC wakiwa nafasi ya pili kwa alama 36 baada ya kucheza mechi 15.

Aidha, Yanga ipo kileleni na alama 40 baada ya mechi sawa na Simba SC huku Azam FC wakiwa na alama 32 nafasi ya tatu wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news