Simba SC yamsamehe Clatous Chama

DAR ES SALAAM-Klabu ya Simba imemsamehe kiungo wake Mzambia, Clatous Chota Chama aliyekuwa amesimamishwa kwa makosa ya kinidhamu.

Desemba 21, 2023 klabu ya Simba ilitoa taarifa za kumsimamisha kiungo huyo kwa utovu wa nidhamu na kwamba suala lake lingeamuliwa na Kamati ya Maadili ya Klabu hiyo.


Taarifa iliyotolewa na Simba leo Februari 2,2024 imesema klabu hiyo imemsamehe Chama baada Kamati ya Ufundi ya Bodi kupitia barua ya Chama. 

Pia, msamaha huo umezingatia uamuzi wa kocha mkuu, Abdelhak Benchikha kumsamehe mchezaji huyo, hivyo suala lake kutofikishwa tena mbele ya Kamati ya Maadili ya Klabu;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news