Simba SC yatinga 32 bora ASFC

DAR ES SALAAM-Simba SC imetinga hatua ya 32 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup baada ya kuifunga Tembo FC kutoka Tabora mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex.
Luis Miqussone aliwapatia bao la kwanza dakika ya 10 kwa shuti kali la chini chini ndani ya 18 baada ya kumalizia pasi iliyopigwa na Fred Michael.

Aidha,Saido Ntibazonkiza aliwapatia bao la pili kwa kichwa dakika ya 31 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Sadio Kanoute.

Kipindi cha pili walirudi kwa kasi na kuliandama lango la Tembo, lakini mlinda mlango wao alikuwa makini kuhakikisha wanakuwa salama.

Saleh Karabaka aliwapatia bao la tatu dakika ya 81 baada ya kupokea pasi ya upendo kutoka kwa Ntibazonkiza.

Dakika moja baadae Pa Omar Jobe aliwapatia bao la nne kwa shuti kali akiwa nje ya 18 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Ntibazonkiza.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news