Ukwasi wa NHC wafikia shilingi trilioni 5.14, Serikali yazidi kuneemeka

DODOMA-Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), hivi sasa lina ukwasi wa shilingi trilioni 5.14, aidha linalipa kodi zote za Serikali kiasi cha shilingi bilioni 35 kwa mwaka.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Hamad Abdallah akionesha moja wapo ya miradi mikubwa zaidi ya NHC wa Morocco Square uliopo jijini Dar es Salaam. Mradi huo unajumuisha vitega uchumi mbalimbali yakiwemo makazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Hamad Abdallah ameyasema hayo wakati akitoa wasilisho lake kwa ujumbe kutoka Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC) uliofanya ziara jijini Dodoma ya siku moja kubadilishana ujuzi wa kiuendeshaji na NHC.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Bw. Hamad Abdallah amesema, NHC inapata faida ya zaidi ya shilingi bilioni 135 kwa mwaka.
Baada ya wasilisho hilo, ujumbe huo kutoka Zanzibar ulipata fursa ya kufanya ziara ya kikazi kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na NHC kama mkandarasi na pia ile ambayo NHC inatekeleza kama miradi yake ya ndani.
Awali akizungumza wakati akiukaribisha uongozi wa ZHC, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa NHC, Dorothy Mwanyika amesema, ushirikiano ulioanzishwa baina ya taasisi mbili hizo ni jambo lenye manufaa makubwa kwa taifa na hivyo taassisi hizo hazina budi kufanya tathmini za mara kwa mara za maendeleo ya ushirikiano.
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC), Bi. Dorothy Mwanyika, akiikaribisha Bodi ya Shirika la Nyumba Zanzibar (NHC), iliyoko Dodoma kwa ziara ya kubadilishana uzoefu.

Hii itasaidia kutambua maeneo ya mafanikio na changamoto na kutoa fursa ya kurekebisha mwelekeo inapohitajika. Ziara hiyo ni mwendelezo wa utekelezaji wa ushirikiano waliousaini miezi kadhaa iliyopita jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Zanzibar ( ZHC), Abdallah Mwinyigogo, akizungumza baada ya ukaribisho kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa bodi ya NHC, Bi Dorothy Mwanyika, jijini Dodoma, ambako Bodi ya ZHC na Menejimenti yake, ipo kwaajili ya ziara ya kubadilishana uzoefu na NHC.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Zanzibar (ZHC), Abdallah Mwinyigogo, amelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa ushirikano wake tangu kuanzishwa kwake na kwamba ushirikano huo umejenga umoja na utayari wa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa mafanikio zaidi ya siku zijazo.
Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa ( NHC), Mkoa wa Dodoma, Bw. Gibson Mwaigomole, akizungumza na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Nyumba la Taifa, Dorothy Mwanyika, katika mradi wa Chamwino, Dodoma, wakati wa ziara ya Bodi ya Shirika la Nyumba la Zanzibar ZHC) na menejimenti yake, katika mradi huo, ikiwa ni sehemu ya ziara ya ZHC, ya kubadilishana uzoefu na NHC.

Serikali zote mbili kwa maana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mashirika hayo yanajengewa uwezo wa kutosha ili kuendelea kutekeleza miradi bora ya makazi kwa ajili ya ustawi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news