Waziri Mkuu asisitiza mpango wa Serikali kuendelea kutumia TEHAMA shuleni

LINDI-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuhakikisha Shule zote nchini zinakuwa na mifumo bora ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kurahisisha ujifunzaji na ufundishaji kwenye ngazi zote za elimu.
Ameyasema hayo leo Alhamisi, Februari 22, 2024 wakati alipotembelea na kukagua miundombinu ya TEHAMA iliyowekwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Lucas Malia, Ruangwa mkoani Lindi.

Akizungumza na wazazi na wanafunzi wa Shule hiyo Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa kwa kuwezesha kufunga mifumo ya TEHAMA katika shule hiyo.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa, amesema Shule hiyo ya Lucas Malia itakuwa kitovu cha ufundishaji kupitia mifumo ya TEHAMA kwa shule za Sekondari Wilayani Ruangwa.

Katika hatua nyingine Mheshimiwa Majaliwa amesema wana Ruangwa wana kila sababu ya kumshukuru Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na manufaa ambayo Wilaya hiyo imepata kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.
"Wana-Ruangwa niwakati wetu wa kujivunia uwepo wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, jukumu lenu ni lilelile la kuniunga mimi mkono nifanye kazi, na kumuunga mkono Rais wetu Dkt. Samia afanye kazi yake vizuri, lazima mjivunie, mumuombee, mumsemee, mumtetee na kumuunga mkono katika kila jambo lake”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news