Wilaya ya Amani kichama yaonesha ubunifu

ZANZIBAR-Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Mkoa wa Mjini kichama Mariam Idd Kireti ameupongeza uongozi wa UWT Wilaya ya Amani kichama kwa kuanzisha Kamati Maalum ya Uchumi na kuleta mabadiliko ya kimaendeleo katika wilaya hiyo.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na wanawake hao huko katika Ukumbi wa Tawi la CCM kwa Wazee Wilaya ya Mjini.

Amesema, Wilaya ya Amani haina vitega uchumi vya kujiendesha hivyo kuwepo kwa kamati hiyo, itaweza kuwa kichocheo cha kuleta maendeleo kwa UWT na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla.

Hivyo ameupongeza uongozi wa UWT wilayani humo kwa kuanzisha kamati hiyo kwani itaweza kunyanyua uchumi na kuleta maendeleo.

Amesema, kamati hiyo, itaweza kukaa pamoja na Kamati Tekelezaji na kupanga mikakati mbalimbali ya kupata miradi ya kiuchumi na kuweza kujiendeleza kiuchumi.

Hata hivyo,amewataka kuacha makundi kwani kuendesha makundi ni kikwazo cha kukwamisha maendeleo dhidi yao.

‘‘Mimi sina Mtu bali ni wa Umoja wa Wanawake hivyo ukiniona Mjini ni Katibu wa Wanawake wa Mjini na Ukiniona Amani ujuwe ni Kiongozi wa Wanawake wa Amani, hapana Mtu wa Mtu, sisi sote ni Watu wa UWT, njooni tufanye kazi za Umoja wetu,’’amesema Katibu Kireti.

Hata hivyo, aliwapongeza madiwani wanawake waliomo katika Wilaya hiyo na kuwaomba kuzidi kusaidiana katika kusimamia UWT katika ngazi za Matawi na Wadi kwani kumekuwa na matatizo madogo madogo.

‘‘Sina shaka na Majimbo, tunakutana mara kwa mara lakini ngazi za Matawi na Wadi, naomba mutusaidie, kazi mnayofanya ni nzuri tangu nilipokuja sijawahi kupata malalamiko ya Madiwani, hongereni sana,’’alipongeza Katibu huyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Amani kichama, Fransisca Clement amesema Wanawake wa Wilaya hiyo wapo tayari wakati wowote iwe Jua au Mvua katika kupambania Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake.

Nao wanawake hao wameahidi kushirikiana na kufanya kazi katika ngazi ya matawi, wadi na Majimbo ili kuzidi kukiimarisha chama sambamba na kutekeleza maagizo waliopewa ikiwemo kufanya maandalizi ya Daftari la kudumu la Wapiga kura awamu ya pili wakati utakapofika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news