Arusha ni salama,wahalifu wakamatwa

NA ABEL PAUL

JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limesema limejipanga vyema kuhakikisha wananchi wanasheherekea Sikukuu ya Pasaka kwa amani na tulivu katika maeneo ya ibada na kumbi za starehe.
Akitoa taarifa hiyo leo Machi 29,2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, SACP Justine Masejo amesema, jeshi hilo limejipanga vyema ili kuhakikisha Ibada ya Pasaka inafanyika katika hali ya amani, utulivu na usalama.

SACP Masejo amesema kuwa, askari watakuwa katika doria za miguu, Pikipiki, Mbwa na magari katika mitaa mbalimbali ya jiji la Arusha na Mkoa kwa ujumla ili kuzuia uhalifu wowote ule.

Pia SACP Masejo amesema kuwa,Jeshi la Polisi Mkoa Arusha limepata taarifa kupitia mitandao ya kijamii ikiwaonyesha vijana wawili wakiwa na pikipiki na kumpora mwanamke mmoja vitu alivyokuwa navyo maeneo ya Burka Kisongo Jijini Arusha.

Kamanda Masejo ameviambia vyombo vya Habari kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo baada ya kupata taarifa hiyo mara moja walianza uchunguzi na kuwatambua wahusika wa tukio hilo ambapo Machi 28,2024 mtuhumiwa Jamal Idd Ramadhan (22) mkazi wa Ngusero alikamatwa na jitihada za kuwatafuta wengine zinaendelea.

Vivile vile Jeshi la Polisi mkoani Arusha limesema linaendelea kuwashukuru wananchi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu Pamoja na waandishi wahabari kwa kufichua uhalifu katika Mkoa huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news